Chuo Cha Ualimu
Paradigms
Africa's Center for
Educational
Excellence!
KAULI YA MWENYEKITI WA BODI
“Nawahamasisha wazazi / walezi/watu binafsi wanaotaka kuwapatia vijana wao au kujipatia elimu bora kuchagua Chuo cha Ualimu Paradigms. Kwetu Paradigms elimu bora ni ile inayomuwezesha mwanafunzi kujijengea uwezo wa kiakili wa kuhoji masuala ya msingi kwa kujiamini kuwa anaweza, huku akithubutu kuchukua hatua mahsusi za kujiletea maendeleo.”
Prof. I. K. Bavu
Kwa nini utuchague sisi:-
Tumedhamiria na tunazo rasilimali sahihi za kutuwezesha kutoa kilicho bora na tumejipanga vizuri kukupa zaidi ya kile unachotegemea.
Rasilimali hizo ni:-
Rasilimali watu:-
Chuo chetu kina wakufunzi 15, wote wakiwa na shahada za vyuo vikuu vinavyotambulika nchini na nje ya nchi, na wafanyakazi 8 wa kada mbali mbali zikiwemo mganga wa shule, nesi, madereva, wapishi, matron, patron. Chuo kiinasimamiwa na bodi yenye wataalam wazoefu katika Uongozi na Utawala. Wataalam hawa wametafutwa, kutahiniwa na kuhamasishwa kutoa huduma bora, kwa wakati na inayokithi matarajio ya wadau / wateja wetu.
Rasilimali zisizohamishika
Chuo kina madarasa ya kisasa, maktaba, maabara na mabweni ya kutosheleza wanachuo 700, ofisi za utawala, nyumba 3 za waalimu, viwanja vya mcihezo mbali mbali, zahanati na duka la shule; vyote vikiwa vimejengwa kwenye eneo la ekari 25 linalomilikiwa na Taasisi yetu.
Aidha chuo kimeunganishwa na umeme wa Tanesco, maji ya Dawasa na barabara inayopitika mwaka mzima pia vipo visima 3 vya maji (deep wells) ambavyo vinatoa maji ya kutosheleza huduma. Tunalo jenereta la kutosheleza mahitaji.
Taasisi inao mpango endelevu wa miaka 10 wa kujenga madarasa 30, mabweni 6, ukumbi / bwalo na jiko, nyumba 12 za waalimu, na uwanja mkubwa wa michezo mbalimbali.
Habari / uelewa
Taasisi kwa kushirikiana na wataalam wake imeandaa sera muafaka zinazotekelezeka, endelevu na zinazokidhi haja za wakati uliopo na ujao zikiainisha bayana wajibu na majukumu ya wadau mbali mbali katika kuwapatia wateja wetu kilicho bora. Taasisi imejiunganisha na wadau mbali mbali kwa njia mbali mbali zikiwemo simu, fax na barua pepe.
Kwa kuwa tunaamini mchango wa wazazi na wadau wote katika kufanikisha elimu ya wanachuo wetu, chuo kinasimamiwa na kamati ya chuo na kamati ndogo ndogo za wazazi hivyo kuwapa fursa ya kufuatilia, kushauri na kuelekeza jambo ambalo linawapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuwapatia vijana wetu elimu bora.
Mtandao na Mahusiano
Chuo, kwa kupitia Taasisi tanzu ya Paradigms Institute Ltd, kimeunganishwa na mitandao mbali mbali, ndani na nje ya nchi inayotoa huduma zinazofanana / landana, na zenye mustakabali mmoja.
Taasisi inao mkakati mahsusi na endelevu wa kutumia mahusiano yaliyopo baina yake na mtandao huu kujipatia rasilimali mahsusi za kuendeleza chuo na Taasisi kwa ujumla. Kwa sasa Paradigms Institute ltd inajivunia uhusiano uliojengwa na bingwa wa uwekezaji nchini, TANZANIA INVESTMENT BANK LTD ambaye ametuwezesha kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kuboresha na kupanua huduma zetu.
Tunalenga na tumedhamiria kuwa Taasisi ya Elimu na Utaalam Uliotukuka.