Chuo Cha Ualimu
Paradigms
Africa's Center for
Educational
Excellence!
KAULI YA MWENYEKITI WA BODI
“Nawahamasisha wazazi / walezi/watu binafsi wanaotaka kuwapatia vijana wao au kujipatia elimu bora kuchagua Chuo cha Ualimu Paradigms. Kwetu Paradigms elimu bora ni ile inayomuwezesha mwanafunzi kujijengea uwezo wa kiakili wa kuhoji masuala ya msingi kwa kujiamini kuwa anaweza, huku akithubutu kuchukua hatua mahsusi za kujiletea maendeleo.”
Prof. I. K. Bavu
Shule ya Sekondari
Sisi ni akina nani?
Shule ya Sekondari Paradigms, ni shule yenye kutoa elimu bora na kuaandaa wanafunzi bora ambao ni mfano wa kuigwa. Shule inatoa elimu na kuandaa wanafunzi kidato cha I – VI. Shule inapokea wanafunzi wa kutwa na bweni, wavulana kwa wasichana.
Tuko wapi?
Shule ya Sekondari Paradigms ipo kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza, katika vilima vya Bonyokwa, Wilayani Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Shule imejengwa na inaendelea kupanuliwa katika eneo la Ekari 25, linalomilikiwa, kupangwa na kuendelezwa na Paradigms Institute Ltd.
Tunafanya nini?
Tunafundisha masomo ya sekondari (I – VI) kulingana na mtaala wa Taasisi ya Elimu ya Taifa (Tanzania Institute of Education) unaotahiniwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Shule ya sekondari Paradigms inafundisha masomo yote kwa wanafunzi wa kidato cha I hadi IV na wanafunzi wa kidato cha V na VI kuna michepuo ya PCM, PCB, PGM, CBG, EGM, ECA, HGE, HGL, HKL, HGK
Kwa nini utuchague sisi
Tumedhamiria na tunazo rasilimali sahihi za kutuwezesha kutoa kilicho bora na tumejipanga vizuri kukupa zaidi ya kile unachotegemea. Rasilimali hizo ni:-
(a) Rasilimali watu:-
Shule yetu ina waalimu 17, wote wakiwa na shahada za vyuo vikuu vinavyotambulika nchini na nje ya nchi, na wafanyakazi 14 wa kada mbali mbali zikiwemo mganga wa shule, nesi, madereva, wapishi, matron, patron. Shule inasimamiwa na bodi yenye wataalam wazoefu katika Uongozi na Utawala. Wataalam hawa wametafutwa, kutahiniwa na kuhamasishwa kutoa huduma bora, kwa wakati na inayokidhi matarajio ya wadau / wateja wetu.
(b) Rasilimali zisizohamishika
Shule ina madarasa ya kisasa, maktaba, maabara na mabweni ya kutosheleza wanafunzi 700, ofisi za utawala, nyumba 3 za waalim, viwanja vya mcihezo mbali mbali, zahanati na duka la shule; vyote vikiwa vimejengwa kwenye eneo la ekari 25 linalomilikiwa na Taasisi yetu.
Aidha shule imeunganishwa na umeme wa Tanesco, maji ya Dawasa na barabara inayopitika mwaka mzima pia vipo visima 3 vya maji (deep wells) ambavyo vinatoa maji ya kutosheleza huduma. Tunalo jenereta la kutosheleza mahitaji.
Taasisi inao mpango endelevu wa miaka 10 wa kujenga madarasa 40, mabweni 6, ukumbi / bwalo na jiko, nyumba 12 za waalimu, na uwanja mkubwa wa michezo mbalimbali.
(c) Habari / uelewa
Taasisi kwa kushirikiana na wataalam wake imeandaa sera muafaka zinazotekelezeka, endelevu na zinazokidhi haja za wakati uliopo na ujao zikiainisha bayana wajibu na majukumu ya wadau mbali mbali katika kuwapatia wateja wetu kilicho bora. Taasisi imejiunganisha na wadau mbali mbali kwa njia mbali mbali zikiwemo simu, fax na barua pepe.
Kwa kuwa tunaamini mchango wa wazazi na wadau wote katika kufanikisha elimu ya wanafunzi wetu, sekondari inasimamiwa na kamati ya shule na kamati ndogo ndogo za wazazi hivyo kuwapa fursa ya kufuatilia, kushauri na kuelekeza jambo ambalo linawapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuwapatia vijana wetu elimu bora.
(d) Mtandao na Mahusiano
Shule, kwa kupitia Taasisi tanzu ya Paradigms Institute Ltd, imeunganishwa na mitandao mbali mbali, ndani na nje ya nchi inayotoa huduma zinazofanana / landana, na zenye mustakabali mmoja.
Taasisi inao mkakati mahsusi na endelevu wa kutumia mahusiano yaliyopo baina yake na mtandao huu kujipatia rasilimali mahsusi za kuendeleza shule na Taasisi kwa ujumla. Kwa sasa Paradigms Institute ltd inajivunia uhusiano uliojengwa na bingwa wa uwekezaji nchini, TANZANIA INVESTMENT BANK LTD ambaye ametuwezesha kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kuboresha na kupanua huduma zetu.
Tunalenga na tumedhamiria kuwa Taasisi ya Elimu na Utaalam Uliotukuka.
ADA YA SEKONDARI NA KIDATO CHA 5 & 6
Kutwa 250,000/= x 3 = 750,000/=
Bweni 450,000 x 3 = 1,350,000/=
Usajili 100,000/= (mara moja tu kwa mwaka)
Ada inalipwa kwa vipindi vitatu vinavyolingana, Januari, Aprili na Julai kwa Sekondari na Machi, June na Octoba kwa kidato cha 5 & 6. Malipo yote yafanyike kupitia benki, Akaunti yetu ni 01J1009183700 Paradigms Secondary School katika tawi lolote la CRDB Bank. Tafadhali ukilipa tuletee pay – in – slip.
Pia taasisi yetu (Paradigms Institute Ltd) tunamiliki shule zifuatazo:-
(i) Shule ya awali Reg. No. DS. 02/7/E.A 091
(ii Shule ya msingi Reg. No. DS. 02/7/091
(iii) Chuo cha ualimu CU 89
Chuo cha ualimu kinatoa kozi zifuatazo:-
(a) Ualimu wa chekechea (shule za awali)
(b) Ualimu wa shule ya msingi (Grade III A)
(c) Ualimu wa sekondari (Diploma in Education)
Kwa mawasiliano zaidi:
Mkuu wa shule
Shule ya Sekondari Paradigms
S.L.P. 53848,
DAR ES SALAAM.
Simu: 0715 758093, 0715 263999, 0716 542462
Barua Pepe: Paradigmsltd@yahoo.co.uk,
maksnr63@gmail,com
Website: www.paradigms.co.tz
Tupo Kimara – Bonyokwa!!!
Bofya hapo chini kuchukua fomu
Fomu ya Kujiunga na High School