Chuo Cha Ualimu

Paradigms

Africa's Center for

Educational

Excellence!

 
`

KAULI YA MWENYEKITI WA BODI

“Nawahamasisha wazazi / walezi/watu binafsi wanaotaka kuwapatia vijana wao au kujipatia elimu bora kuchagua Chuo cha Ualimu Paradigms. Kwetu Paradigms elimu bora ni ile inayomuwezesha mwanafunzi kujijengea uwezo wa kiakili wa kuhoji masuala ya msingi kwa kujiamini kuwa anaweza, huku akithubutu kuchukua hatua mahsusi za kujiletea maendeleo.”

Prof. I. K. Bavu

 
 
 
 
Albamu ya Picha za Shule
Angalia picha za shule yetu. Bofya picha inayotiririka hapa chini uweze kupata picha zaidi.
 
 
 
Shule ya Msingi

Sisi ni akina nani?


Shule ya awali na msingi Paradigms, ni shule yenye kutoa elimu bora na kuaandaa wanafunzi bora ambao ni mfano wa kuigwa.

Shule inapokea wanafunzi wa kutwa na bweni, wavulana kwa wasichana.

Tuko wapi?


Shule ya awali na msingi Paradigms ipo kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza, katika vilima vya Bonyokwa, Wilayani Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Shule imejengwa na inaendelea kupanuliwa katika eneo la Ekari 25, linalomilikiwa, kupangwa na kuendelezwa na Paradigms Institute Ltd.

Masomo yatolewayo:


Tunafundisha masomo yafuatayo:-
Hisabati, sayansi, Haiba, Tehama, Kiswahili, Kiingereza, Jiografia, Historia, Uraia, Stadi za kazi, Kifaransa na “Computer”

 

TUNAMILIKI NA KUENDESHA SHULE ZIFUATAZO:

 

Shule ya awali; Paradigms (Nursery School) REG. no. DS.O2/7/E.A 091

 Shule ya Msingi; Paradigms (Primary School) REG. no. DS.02/7/091

Shule ya sekondari; Paradigms Form I------VI. REG. NO. 2539

 

TUNAFUNDISHA MICHEPUO IFUATAYO KIDATO CHA TANO NA SITA

PCM, PCB, CBG, PGM, EGM, HGE, HKL, HGK&HGL

 Chuo cha Ualimu ngazi ya Diploma, daraja la III A na Elimu ya awali CU 89

 

Kwa nini utuchague sisi:-


Tumedhamiria na tunazo rasilimali sahihi za kutuwezesha kutoa kilicho bora na tumejipanga vizuri kukupa zaidi ya kile unachotegemea.  Rasilimali hizo ni:-

 (a)     Rasilimali watu:-
Shule zetu zina waalimu 26, 20 kati yao wakiwa na shahada za ualimu toka vyuo vikuu na uzoefu katika fani ya ufundishaji, wote wakiwa na shahada za vyuo vikuu vinavyotambulika nchini na nje ya nchi, na wafanyakazi 8 wa kada mbali mbali zikiwemo mganga wa shule, nesi, madereva, wapishi, matron, patron.  Shule zinasimamiwa na bodi yenye wataalam wazoefu katika Uongozi na Utawala.  Wataalam hawa wametafutwa, kutahiniwa na kuhamasishwa kutoa huduma bora, kwa wakati na inayokidhi matarajio ya wadau / wateja wetu.

(b)      Rasilimali zisizohamishika
Shule zina madarasa ya kisasa, maktaba, maabara na mabweni ya kutosheleza wanafunzi 700, ofisi za utawala, nyumba 3 za walimu, viwanja vya mcihezo mbali mbali, zahanati na duka la shule; vyote vikiwa vimejengwa kwenye eneo la ekari 25 linalomilikiwa na Taasisi yetu.

Shule zimeunganishwa na umeme wa Tanesco, maji ya Dawasa na barabara inayopitika mwaka mzima pia vipo visima 3 vya maji (deep wells) ambavyo vinatoa maji ya kutosheleza huduma.  Tunalo jenereta la kutosheleza mahitaji.
Taasisi inao mpango endelevu wa miaka 10 wa kujenga madarasa 30, mabweni 6, ukumbi / bwalo na jiko, nyumba 12 za waalimu, na uwanja mkubwa wa michezo mbalimbali.

(c)       Habari / uelewa
Taasisi kwa kushirikiana na wataalam wake imeandaa sera muafaka zinazotekelezeka, endelevu na zinazokidhi haja za wakati uliopo na ujao zikiainisha bayana wajibu na majukumu ya wadau mbali mbali katika kuwapatia wateja wetu kilicho bora.  Taasisi imejiunganisha na wadau mbali mbali kwa njia mbali mbali zikiwemo simu, fax na barua pepe.
Kwa kuwa tunaamini mchango wa wazazi na wadau wote katika kufanikisha elimu ya wanachuo  wetu, chuo kinasimamiwa na kamati ya chuo na kamati ndogo ndogo za wazazi hivyo kuwapa fursa ya kufuatilia, kushauri na kuelekeza jambo ambalo linawapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuwapatia vijana wetu elimu bora.

(d)      Mtandao na Mahusiano
Shule, kwa kupitia Taasisi tanzu ya Paradigms Institute Ltd, imeunganishwa na mitandao mbali mbali, ndani na nje ya nchi inayotoa huduma zinazofanana / landana, na zenye mustakabali mmoja. 

Taasisi inao mkakati mahsusi na endelevu wa kutumia mahusiano yaliyopo baina yake na mtandao huu kujipatia rasilimali mahsusi za kuendeleza chuo na Taasisi kwa ujumla.  Kwa sasa Paradigms Institute ltd inajivunia uhusiano uliojengwa na bingwa wa uwekezaji nchini, TANZANIA INVESTMENT BANK LTD ambaye ametuwezesha kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kuboresha na kupanua huduma zetu.

Tunalenga na tumedhamiria kuwa Taasisi ya Elimu na Utaalam Uliotukuka

Gharama za shule;

 

Shule ina Mihula mitatu. Gharama hizi hapa chini hulipwa kila muhula.

 

A.   Shule ya Msingi


KARO / ADA
Shule ina mihula mitatu.  Gharama hapa chini hulipwa kila mwanzoni mwa muhula

KUTWA      Ada         230,000/= x 3   =      690,000/=
BWENINI    Ada       380,000/= x 3   =   1,140,000/=

Gharama za awali za kujiunga na shule = 100,000/= (hulipwa mara moja tu)

 

NB:     Gharama zikishatolewa hazitarudishwa kwa sababu yeyote ile.  Kanuni za shule na masharti mengine utayakuta shuleni Gharama hizi zilipwe kwenye Acc. Na. 01J1096071400; Paradigms Primary School, kwenye benki yeyote ya CRDB Bank PLC, na uje na pay in slip shuleni ili upate risiti.

 

Wasiliana nasi sasa:-


Mwalimu Mkuu
Paradigms Nursary and Primary School
S.L.P. 53843 Dar es Salaam
Simu: 0715 744999, 0715 263999
Barua Pepe:  Paradigmsltd@yahoo.co.uk,
maksnr63@gmail,com
Website:  www.paradigms.co.tz

Tupo Kimara – Bonyokwa!!!

 

Jipatie Maelekezo na Fomu Ya Kujiunga Na Shule ya Msingi

Bofya hapo chini kuchukua fomu utakayo

Fomu ya hule ya Msingi