Chuo Cha Ualimu
Paradigms
Africa's Center for
Educational
Excellence!
KAULI YA MWENYEKITI WA BODI
“Nawahamasisha wazazi / walezi/watu binafsi wanaotaka kuwapatia vijana wao au kujipatia elimu bora kuchagua Chuo cha Ualimu Paradigms. Kwetu Paradigms elimu bora ni ile inayomuwezesha mwanafunzi kujijengea uwezo wa kiakili wa kuhoji masuala ya msingi kwa kujiamini kuwa anaweza, huku akithubutu kuchukua hatua mahsusi za kujiletea maendeleo.”
Prof. I. K. Bavu
Paradigms
Inasomeka paradaimz
Ina maana ya mfano bora (a model / pattern)
Sisi ni akina nani?
Chuo cha ualimu Paradigms, ni chuo chenye kutoa elimu bora na kuaandaa walimu bora ambao ni mfano wa kuigwa. Chuo kinatoa elimu na kuandaa walimu ngazi ya Stashahada, Cheti cha Daraja la 3 A na cheti cha Ualimu wa awali. Chuo kinapokea wanachuo wa kutwa na bweni, wavulana kwa wasichana.
Tuko wapi?
Chuo cha Ualimu Paradigms kipo kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza, katika vilima vya Bonyokwa, Wilayani Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Chuo kimejengwa na kinaendelea kupanuliwa katika eneo la Ekari 25, linalomilikiwa, kupangwa na kuendelezwa na Paradigms Institute Ltd.
Tunafanya nini?
Tunafundisha masomo ya ualimu kulingana na mtaala wa Taasisi ya Elimu ya Taifa (Tanzania Institute of Education) unaotahiniwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).