Africa's Center for
Educational
Excellence!
BOARD CHAIRMAN’S STATEMENT
“I recommend/urge parents, guardians and individual persons looking for quality education for their children or self, to choose Paradigms Teacher’s Training College. To us, quality education is the education that produces inquiring mind that guides self development.”
Prof. I. K. Bavu
Nursery School
Paradigms Nursery and Primary School
Mchanganuo wa ada, maelekezo, kanuni na sheria za shule kwa mwaka 2010.
Malipo ya awali: Hulipwa mara moja tu wakati wa usajili
Maombi ya usajili 5,000/=
Usajili 15,000/=
Fedha za tahadhari 20,000/=
Sare za shule 30,000/=
Fedha za matibabu 30,000/=
Jumla 100,000/=
Ada ya shule (karo): Hulipwa kwa awamu tatu
Jumla ya karo yote:
(i) Bweni 1,140,000/= kwa miezi mitatu
(ii) Kutwa 690,000/= kwa miezi mitatu
Mchanganuo wa vipindi vya malipo:
Payment instalments:
|
JANUARI |
MEI |
SEPTEMBA |
JUMLA |
Bweni |
380,000/= |
380,000/= |
380,000/= |
1,140,000/= |
Kutwa |
230,000/= |
230,000/= |
230,000/= |
690,000/= |
USAFIRI: Hulipwa mara moja kila miezi mitatu
Kanda A: 30,000/= x 3 = 90,000/=
Kanda B: 45,000/= x 3 = 135,000/=
Mchanganuo wa vipindi vya malipo
ZONE |
JANUARI |
MEI |
SEPTEMBA |
JUMLA / MWAKA |
Kanda A |
90,000/= |
90,000/= |
90,000/= |
270,000/= |
Kanda B |
135,000/= |
135,000/= |
135,000/= |
405,000/= |
SHULE ILIKO:
Shule iko Bonyokwa, kata ya kimara, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam; km 3.5 kusini mwa barabara ya Morogoro.
Namna ya kufika:
(i) Kimara mwisho:
Fika Kimara mwisho, utaona kibao chetu, fuata barabara hiyo. Endapo unatumia usafiri wa umma, panda magari yaendayo Bonyokwa, ukifika kituo cha mwisho, utaona kibao chetu, shule iko karibu.
(ii) Suca
Fika Kimara Suca. Fuata barabara iendayo Golani, ufikapo utaona kibao chetu.
Endapo unatumia usafiri wa uma, panda gari suca, shuka kijiweni, fuata kibao chetu, utafika shuleni ni karibu sana.
MAELEKEZO MUHIMU WAKATI WA KUJIUNGA:
1. Uwe umelipa karo yote ya awamu husika.
2. Karo na fedha za usajili ziwe zimelipwa kwenye Benki ya CRDB; kwa jina: Paradigms Primary School; Na. ya Akaunti 01J0196071400 kwenye tawi lolote nchini; na uje na stakabadhi halisi ya malipo benki “Bank Pay in Slip” na siyo nakala. Hatupokei fedha taslimu wala hundi.
3. Uwe umesoma na kuelewa kanuni na sheria za shule na kusaini kukubaliana nazo (Hati No. 5)
4. Uwe umejaza kwa usahihi hati No.1 ya uthibitisho wa usajili wa mwanafunzi.
5. Uwasilishe hati ya uthibitisho wa afya ya mwanao (hati No. 3), ukiambatanisha vyeti muhimu endapo mwanao ana mahitaji maalum, au ugonjwa unaompata mara kwa mara.
6. Ulete vitu / vifaa vyote vilivyoelekezwa katika hati ya mahitaji binafsi ya mwanafunzi (Hati No. 4).
7. Hakikisha umepata stakabadhi halisi na halali ya kila malipo na umefananishwa kiwango cha ada iliyobaki baada ya malipo uliyofanya na wakati wa kulipa.
8. Hakikisha umemkabidhi mwanao kwa mwalimu husika au mtu mwingine mwenye dhamana hiyo kabla hujaondoka shuleni.